3 Aprili 2023 - 14:59
Putin: Uhusiano wa Russia na Belarus unaimarika licha ya mashinikizo ya Magharibi

Rais wa Russia amemhutubu Rais wa Belarus akisema: uhusiano wa Russia na Belarus unazidi kuimarika kuliko ikilinganishwa na huko nyuma licha ya vikwazo vya Magharibi. Rais Vladimir Putin wa Russia amebainisha hayo katika ujumbe wa pongezi aliomtumia Rais wa Belarus kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Muungano wa Moscow na Minsk.

Katika ujumbe wake huo wa pongezi kwa Rais Alexander Lukashenko wa Belarus, Rais Vladimir Putin wa Russia amebainisha kuwa: Moscow na Minsk zinafanya juhudi kubwa katika uga wa kimataifa na kuhusu masuala ya ulinzi licha ya vikwazo vya magharibi dhidi yazo; na zinatekeleza mipango mbalimbali kwa lengo la kuimarisha mamlaka za kitaifa, uchumi, sayansi na teknolojia.  

Vladimir Putin amesisitiza pia kuwa Russia na Belarus zinapanua kwa utaratibu ushirikiano wa wenye maslahi kati ya pande mbili. Rais wa Russia ameeleza matumaini yake kuwa, ushirikiano wa wananchi wa Belarus na Russia utaongezeka katika siku zijazo. 

Jumamosi iliyopita Rais wa Russia alitangaza kuwa Moscow inapeleka sehemu ya silaha zake za nyuklia  huko Belarus ikiwa ni katika kujibu kuongezeka hatua za kijeshi za nchi za Magharibi na uungaji mkono mkubwa wa nchi hizo kwa jeshi la Ukraine. 

Wakati huo huo Rais Alexander Lukashenko wa Belarus na viongozi wa nchi hiyo wameunga mkono kutumwa nchini humo silaha za nyuklia za Russia na kueleza kuwa; silaha hizo zitailinda Belarus dhidi ya vitisho vya Magharibi.  

342/